Kuchakulo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuchakulo ni wanyama wadogo kama kindi katika kabila Xerini la familia Sciuridae. Tofauti na kindi, ambao huishi mitini, kuchakulo huishi ardhini. Wanatokea maeneo makavu ya Afrika, isipokuwa kuchakulo makucha-marefu anayetokea Asia ya Kati. Hula mbegu, makokwa, matunda, matumba, manyasi, machipukizi na wadudu. Huchimba vishimo ambamo walala na kukingwa dhidi ya joto na wanyama mbua. Hutafuta chakula wakati wa mchana.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kuchakulo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kuchakulo miraba (Euxerus erythropus) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 5, spishi 6:
| ||||||||||||||||
Funga