![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/24/Kool_G_Rap_%2528cropped%2529.jpg/640px-Kool_G_Rap_%2528cropped%2529.jpg&w=640&q=50)
Kool G Rap
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nathaniel Thomas Wilson (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Kool G Rap, kwa kifupi G Rap, Kool G. Rap, na Giancana, iliyo maana ya kifupisho "G."; amezaliwa 20 Julai 1968[1]) ni rappa, kutoka mjini Corona jirani na mji wa Queens, New York huko nchini Marekani.[2] Ameanza shughuli zake za kurap katikati mwa miaka ya 1980 akiwa kama nusu ya kundi la Kool G Rap na DJ Polo na pia akiwa kama mwanachama wa Juice Crew.
Kool G Rap | |
---|---|
![]() | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nathaniel Thomas Wilson |
Amezaliwa | 20 Julai 1968 (1968-07-20) (umri 55) Queens, New York City, U.S. |
Asili yake | Corona, Queens, New York City, U.S. |
Aina ya muziki | Hip hop, mafioso rap, hardcore hip hop |
Kazi yake | Rapa, mtayarishaji wa rekodi, mwandishi-skrini, mtunzi wa vitabu |
Miaka ya kazi | 1986–hadi sasa |
Studio | Cold Chillin'/Warner Bros. Records Cold Chillin' Cold Chillin'/Epic Street/SME Records KOCH' |
Ame/Wameshirikiana na | DJ Polo, Juice Crew, Marley Marl, Big Daddy Kane, Rakim, Canibus, Five Family Click, Wu-Tang Clan, Nas, MF Grimm, Mobb Deep, R.A. The Rugged Man, Ras Kass, DJ Premier, Rick Ross |
Mara kwa mara huhesabiwa kama miongoni mwa Ma-MC wenye athira na maarifa ya juu wa muda wote[3][4][5][6][1][7][8]akiwa kama mwanzilishi wa staili ya mafioso rap/street/hardcore[5][9][10][11][12][13] na uimbaji wa silabinyinginyingi.[14] Kwenye albamu yake ya The Giancana Story, ameeleza ya kwamba herufi "G" katika jina lake humaanisha "Giancana" (kajipa jina la jambazi sugu Sam Giancana), lakini kwa namna nyingine mwenyewe eti anadai lina-maanisha "Genius".[1]
Pia amewahi kutajwa na wasanii maarufu wa hip hop kama vile Eminem, Nas, Jay Z, Big Pun, RZA na wengine wengi tu.[15][16][17]