![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/da/DJ_Premier.jpg/640px-DJ_Premier.jpg&w=640&q=50)
DJ Premier
From Wikipedia, the free encyclopedia
Christopher Edward Martin (amezaliwa tar. 21 Machi 1966[1]) ni mtayarishaji wa rekodi na DJ kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama DJ Premier, na mtengenezaji wa muziki wa kundi la watu wawili Gang Starr, akiwa pamoja na rapa/mwimbaji Guru.
DJ Premier | |
---|---|
![]() | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Christopher Edward Martin |
Amezaliwa | 21 Machi 1966 (1966-03-21) (umri 58) Houston, Texas, Marekani |
Asili yake | Houston, Texas, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Mtayarishaji wa rekodi, DJ |
Ala | Drum machine Kinanda Sampler Turntable |
Miaka ya kazi | 1987–mpaka sasa |
Studio | Wild Pitch/EMI (1987–1990) Chrysalis/EMI (1991–1998) Virgin/EMI (1998–2003) Year Round (2003–) |
Kiasili anatokea mjini Houston, lakini ameishi zaidi mjini Brooklyn, New York, kwa ajili ya shughuli zake za kitaalamu. Premier anatazamika kama ndiye mbunifu kwa staili ya "hardcore East Coast hip-hop inayojulikana sana kwa ngoma zake nzito na michano."[2]
Gazeti la The Source limempa jina DJ Premier kuwa kama mmoja kati ya watayarishaji watano wakubwa wa muziki wa hip hop katika historia, wakati wahariri wa About.com wamempa cheo cha #1 katika orodha ya watayarishaji Bora-50.[3]