Big Pun
From Wikipedia, the free encyclopedia
Christopher Rios (9 Novemba 1971 - 7 Februari 2000) alikuwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Big Punisher au Big Pun. Huyu alikuwa Mpuerto Rico-Mwamerika na alianza kupata umaarufu mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1990 akiwa mjini The Bronx.
Big Pun | |
---|---|
![]() | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Christopher Rios |
Amezaliwa | (1971-11-09)9 Novemba 1971 |
Asili yake | South Bronx, Bronx, New York City, New York, Marekani |
Amekufa | 7 Februari 2000 (umri 28) |
Aina ya muziki | Hip hop |
Miaka ya kazi | 1991ā2000 |
Studio | Loud Records |
Ame/Wameshirikiana na | Terror Squad, Cuban Link, Triple Seis, D.I.T.C., Brandy, Remy Ma |
Huyu ni mmoja kati ya waanzilishi wa kundi la muziki wa hop hop la Terror Squad. Alianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika albamu ya The Beatnuts, kwenye nyimbo ya "Off the Books", na katika albamu ya pili ya Fat Joe ya Jealous One's Envy, tena kwenye wimbo wa "Watch Out", alioimba kwa mara ya kwanza akiwa kama msanii wa kujitegemea kufanyakazi na studio ya Loud Records.
Juhudi zake katika muziki zilikujakwisha katika mwaka wa 2000 akiwa na umri wa miaka 28. Big Pun alikufa kwa shinikizo la moyo. Bwana huyu ameacha mke, Liza Rios, na watoto watatu. Anakadiriwa kuwa alifariki akiwa na uzito wa paundi 700 ambazo ni sawa na kilogramu 300. Kila kitu kuanzia kuoga na kuvaa hadi viatu, alikuwa akisaidiwa kufanya shauri ya uzito mkubwa aliokuwa nao.