From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia (kwa Kiamhara የኢትዮጵያ:ኦርቶዶክስ:ተዋሕዶ:ቤተ:ክርስቲያን, Yäityop'ya ortodoks täwahedo bétäkrestyan) ni madhehebu ya dini ya Ukristo iliyotawala watu wa jamii ya Waamhara kwa karne kadhaa hadi sasa.
Wakristo hao wanaotaka kuzingatia imani sahihi ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Ethiopia na Eritrea[1].
Kwa sasa ni kubwa zaidi duniani kuliko mengine yote ya jamii ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, likiwa na waumini milioni 45-50.[2] wengi wao wakiishi nchini Ethiopia,[3] lakini pia Mashariki ya Kati, Ulaya na Amerika.
Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia linaendeleza ushirika na Kanisa la Misri tangu lilipoanzishwa na mtakatifu Frumensyo aliyetumwa na mtakatifu Atanasi, Patriarki wa Aleksandria katikati ya karne ya 4 BK.
Hata hivyo mwaka 1959 lilikubaliwa liwe na Patriarki wake mwenyeji na kujiongoza.
Kufuatana na mapokeo ya huko Misri, Epifania na Pasaka ni sikukuu muhimu sana, na husherehekewa kwa kufanya mambo kama vile kufunga kula na kucheza.
Pia kuna siku kadhaa katika mwaka ambapo ni mboga za majani pekee na samaki ndio huruhisiwa kuliwa.
Ndoa huweza kuanzishwa au kupangwa wakati mwanamume ana umri wa miaka kumi na..., au ishirini na... Kiutamaduni, wasichana wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18, lakini katika karne ya 20, mambo yamebadilika, hivyo sasa umri mdogo kuliko wote wa kuolewa ni miaka 18, na suala hili linasimamiwa na serikali. Ndoa za kiserikali ni nyingi japo pia, wapo watu wanaofunga ndoa katika makani mbalimbali. Na baada ya kufunga ndoa kanisani, suala la talaka halipo na haliwezekani. Kila familia hufanya sherehe ya ndoa baada ya harusi.
Tangu kuzaliwa, padri hutembelea familia kwa ajili ya kumbariki mtoto, na pia kutahiri mtoto kama ni wa kiume. Mama wa mtoto, hutakiwa kukaa ndani kwa siku 40 baada ya kujifungua kama mtoto ni wa kiume na kukaa ndani kwa siku 80 kwa mtoto ni wa kike kabla ya kwenda kanisani kwa ajili ya ubatizo.
Sanaa ya nchini Ethiopia kwa ujumla imeegamia katika masuala ya dini na michoro ya dini.
Mmoja kati ya michoro mizuri zaidi ya vitu au watu wenye macho makubwa na mara nyingi huwa ni watu wanaohusiana na Biblia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.