Juan Diego
From Wikipedia, the free encyclopedia
Juan Diego Cuauhtlatoatzin, yaani Yohane Diego Anayesema-kama-tai, (1474 hivi - 30 Mei 1548) ni mtu wa Mexico maarufu hasa kwa kusadikiwa kwamba alitokea na Bikira Maria akiwa na sura ya chotara. Njozi hiyo ilifuatwa haraka sana na wongofu wa Wahindi Wekundu milioni 8 wa nchi hiyo ambao waliingia Ukristo kati ya mwaka 1532 na 1538.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mwaka 1990, halafu 2002 akamtangaza mtakatifu, wa kwanza kati ya wakazi wa asili ya Amerika.