Bikira Maria wa Guadalupe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bikira Maria wa Guadalupe ni jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na kijiji cha Guadalupe katika nchi ya Meksiko, kilichopata umaarufu kutokana na njozi tano za Bikira Maria kwa Juan Diego mnamo Desemba 1531 zilizosababisha wananchi milioni nane kwa muda mfupi wajiunge na Ukristo.
Basilika lililojengwa mahali hapo linatembelewa na Wakatoliki wengi kuliko patakatifu pengine popote[1][2].
Kumbukumbu yake huadhimishwa tarehe 12 Desemba[3].