Joel Nkaya Bendera
From Wikipedia, the free encyclopedia
Joel Nkaya Bendera (* 30 Mei 1950 + 6 Desemba 2017) alikuwa mwanasiasa na Mbunge katika Bunge la Tanzania.
Bendera alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika miaka ya 1980 [1].
Aliingia katika siasa kama mbunge wa Korogwe akawa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika serikali ya Mizengo Pinda[2].
Alihudumia kama Mkuu wa Mikoa ya Morogoro na Manyara. Mwezi wa Oktoba 2017 alistaafishwa na rais John Magufuli akaendelea kuwa mbunge wa Tanga hadi kifo chake[3].