From Wikipedia, the free encyclopedia
Jimbo Katoliki la Musoma (kwa Kilatini "Dioecesis Musomensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Eneo lake ni la kilometa mraba 25,150 (Mkoa wa Mara isipokuwa wilaya ya Bunda na parokia mbili katika wilaya ya Musoma vijijini) na lina wakazi 1,040,000, ambao kati yao Wakatoliki ni 215,000 (20.7 %). Parokia ziko 30.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Mwanza.
Askofu wake ni Michael George Mabuga Msonganzila na makao yake ni Musoma mjini. Kanisa kuu limejengwa kwa heshima ya Mtume Paulo.
Anasaidiwa na mapadri 58, ambao kati yao 38 ni wanajimbo na 20 ni watawa. Kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 3,707. Pia kuna mabruda 12 na masista 200.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Musoma kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.