kata ya Mbeya, Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Iwambi ni kata ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Iko kati ya Iyunga na Mbalizi kando ya barabara kuu inayoelekea Vwawa na Zambia.
Kata ya Iwambi | |
Mahali pa Iwambi katika Tanzania |
|
Majiranukta: 8°53′24″S 33°25′48″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mbeya |
Wilaya | Mbeya Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 19,798 |
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 19,798 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,387 [2] walioishi humo.
Msimbo wa posta ni 53115.
Iwambi ni kata ambayo kihistoria walipatikana kabila la Wasafwa ambao waliongea lugha yao ya Kisafwa pia waliongozwa na mwene Mpoli ambaye alifariki mwaka 2005 na alizikwa ndani ya Iwambi katika mtaa wa Ivwanga.
Kati ya wenyeji mashuhuri wa Iwambi ni John Butler Walden (1939 – 2002) aliyekuwa kiongozi mmojawapo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakati wa Vita vya Kagera dhidi ya Uganda. Kaburi lake linapatikana Iwambi.
Katika kata ya Iwambi kuna shule mbili za msingi ambazo ni shule ya msingi Iwambi ipo katika mtaa wa Mayombo na shule ya msingi Iyunga ipo katika mtaa wa Isoko. Pia KUna shule moja ya sekondari Iwambi iliyoanzishwa mwaka 2006 chini ya uongozi wa rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.