Isabel dos Santos
Mfanyabiashara mwanamke wa Angola / From Wikipedia, the free encyclopedia
Isabel dos Santos (amezaliwa 1973) ni mfanyabiashara na mjasiriamali wa kike kutoka nchini Angola. Yeye ni mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos, ambaye alitawala nchi hiyo tangu mwaka 1979 hadi 2017. [4] [5]
Isabel dos Santos | |
---|---|
Isabel dos Santos mnamo 2019 | |
tarehe ya kuzaliwa | 20 Aprili 1973 (1973-04-20) (umri 51)[1] |
utaifa | Russia[2], Angola |
ndoa | Sindika Dokolo, tangu 2002 |
watoto | 3[3] |
makazi | Dubai, UAE |
mhitimu wa | King's College London |
taaluma | Mjasiriamali, mfanyabiashara |
Mnamo mwaka 2019 alitajwa kuwa mwanamke tajiri zaidi kwenze bara la Afrika[6]. Mnamo 2013, kulingana na Forbes, jumla ya utajiri wake ilikuwa imezidi dolar za Kimarekani bilioni 2, hivyo alikuwa bilionea wa kwanza wa kike wa Afrika. Forbes alielezea jinsi dos Santos alivyopata utajiri wake kwa kuchukua hisa katika kampuni zinazofanya biashara nchini Angola, na kupendekeza kuwa utajiri wake unatokana kabisa na nguvu za kisiasa ya familia yake. [7] Mnamo Novemba 2015, BBC ilimtaja dos Santos kama mmoja wa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. [8]
Tangu mwaka 2018 serikali ya Angola ilikuwa ikijaribu kumshtaki Isabel dos Santos kwa jinai za ufisadi zilizochangia kwenye mzozo wa uchumi wa Angola katika miaka iliyotangulia. Lakini Isabel hakurudi tena Angola akibaki Ureno. [9]
Mnamo Desemba 30, 2019, Mahakama ya Mkoa wa Luanda iliagiza kufungiwa kwa akaunti zake kwenye benki za Angola na kukamatwa kwa hisa zake katika kampuni pamoja na Unitel na Banco de Fomento Angola. [10] Tangu kuchunguliwa nchini Ureno pia amehamia UAE kama nchi yake rasmi ya kuishi. [11] [12] [13]
Mnamo Januari 11, 2020, serikali ya Angola ilitangaza kwamba inachukua hatua za kisheria za kunyakua mali za dos Santos nchini Ureno [14].