![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e7/Instagram_logo_2016.svg/langsw-640px-Instagram_logo_2016.svg.png&w=640&q=50)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Instagram ni mtandao wa kijamii unaoruhusu mtumiaji kupata huduma ya kushirikisha picha za kawaida na za video mtandaoni.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e7/Instagram_logo_2016.svg/150px-Instagram_logo_2016.svg.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2a/Instagram_logo.svg/105px-Instagram_logo.svg.png)
Programu hii hutumika katika simu aidha za iPhone au mfumo uendeshaji wa Android. Programu inakupa fursa ya kuchukua picha na video, na kuzipitisha katika vichujio vyake ili itakate na kisha kuishirikisha na wale wanaokufuata. Vilevile inakupa fursa ya kushirikisha na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, JamiiTalk, Tumblr na Flickr.[1]
Mtandao huo uliundwa na Kevin Systrom na Mike Krieger na kutolewa rasmi tarehe 6 Oktoba 2010. Hivi sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook baada ya kununuliwa kwa dola za Kimarekani bilioni 1 Aprili 2012.
Baada ya kuanzishwa mwaka 2010, Instagram ilipata umaarufu mkubwa na kupata watumiaji milioni moja ndani ya miezi miwili, milioni 10 ndani ya mwaka mmoja na milioni 800 hadi Septemba 2017. Hadi Oktoba 2015 kulikuwa na picha bilioni 40 toka kwa watumiaji.