From Wikipedia, the free encyclopedia
Facebook ni mtandao wa kijamii unaoruhusu watu kuungana na marafiki, familia, na watu wengine duniani kote. Ilizinduliwa mnamo mwaka 2004 na Mark Zuckerberg na wenzake katika Chuo Kikuu cha Harvard.
Facebook inaruhusu watumiaji kutuma ujumbe, kushiriki picha na video, na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja. Watumiaji wanaweza kuunda kurasa binafsi, kuanzisha makundi, na kufuatilia kurasa za watu au makampuni wanayopenda. Pia wanaweza kushiriki au kutoa maoni au kupenda machapisho, na kushirikishana na wengine maisha yao ya kila siku[1].
Ingawa Facebook ilianza kama jukwaa la wanafunzi wa vyuo vikuu, ilikua haraka na kuwa mmoja kati ya mitandao mikubwa zaidi ya kijamii duniani, ikiwa na mamilioni ya watumiaji. Hata hivyo, kuna maoni tofauti juu ya Facebook, yakiwa ni pamoja na masuala ya faragha na usalama wa data. Baadhi ya watu wanapenda kutumia Facebook kwa kuungana na wapendwa wao, lakini wanaweza pia kuwa na wasiwasi kuhusu jinsi data zao zinavyotumika.