Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
eneo la urithi wa dunia nchini Tanzania, Afrika Masharik / From Wikipedia, the free encyclopedia
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (awali: Selous, matamshi: "saluu") ni hifadhi ya taifa kubwa kuliko yote nchini Tanzania, pia ni kati ya hifadhi ya wanyama kubwa kabisa duniani. Hifadhi imeanzishwa mwaka wa 2019; kabla ya kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi, ilikuwa pori tengefu lililojulikana kwa jina la Selous.
Eneo lake ni la km² 54,600 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Eneo hilo ni kubwa kushinda nchi 70 duniani ikikadiriwa kuwa na eneo sawa na nchi ya Kostarika (Amerika ya Kati) na takribani mara mbili kuliko nchi ya Ubelgiji (Ulaya).
Sehemu kubwa ya eneo iko katika hali ya asili bila kuvurugwa na shughuli za binadamu. Tangu mwaka 1982 imeingizwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia. Tena mwezi Juni 2014 imeingizwa kwenye orodha ya UNESCO ya hifadhi zenye hatari ya kupotewa na uhai wake.