Galula
From Wikipedia, the free encyclopedia
Galula ni kata ya Wilaya ya Songwe katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53831.
Galula iko kwenye Mto Songwe, umbali wa takriban kilomita 18 kutoka Ziwa Rukwa upande wa kusini-mashariki.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,076 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,440 [2] walioishi humo.
Tabaka la mwamba linaloenea kutoka upande wa kusini wa Ziwa Rukwa hadi karibu na Ziwa Nyassa linaitwa "Tabaka la Galula" (kwa Kiingereza Galula formation). Ndani ya tabaka hilo visukuku vingi vimepatikana pamoja na mifupa ya dinosauri wawili, Rukwatitan bisepultus[3] na Mnyamawamtuka moyowamkia [4].