Ferdinando III wa Castilla
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ferdinando III (aliyeitwa kwa Kihispania el Santo, yaani "mtakatifu"; 1199/1201[1][2][3] – 30 Mei 1252) alikuwa mfalme wa Castilla tangu mwaka 1217, wa León tangu mwaka 1230 na wa Galicia tangu mwaka 1231.[4]
Mtoto wa Alfonso IX wa León na wa Berenguela wa Castilla, aliunganisha moja kwa moja falme hizo mbili na kufaulu kuliko wote waliomtangulia katika kurudisha Hispania kusini kwa Wakristo, ikiwemo miji ya Córdoba na Seville.
Pamoja na kufanya bidii kueneza imani, alitawala kwa busara, akistawisha sanaa na sayansi.
Ferdinando III alitangazwa na Papa Klementi X kuwa mtakatifu mwaka 1671.