From Wikipedia, the free encyclopedia
Chuo Kikuu cha Pittsburgh ni chuo cha kiutafiti cha umma nchini Marekani. Jina la Kiingereza ni University of Pittsburgh, na kinaitwa kwa kifupi Pitt. Kiko mji wa Pittsburgh, jimbo la Pennsylvania. Pitt ina jengo maarufu linaloitwa “Cathedral of Learning,” au Jumba Kuu la Ujuzi kwa Kiswahili, ambalo ni jengo la mbili kwa urefu la elimu duniani. Pitt kina kampasi mbalimbali. Hizi Kampasi zipo mahali mbalimbali, pia.
Chuo Kikuu cha Pittsburgh | |
---|---|
University of Pittsburgh | |
Wito | Veritas et Virtus (Kilatini) |
Wito kwa Kiswahili | Ukweli na Wema |
Kimeanzishwa | 1787 |
Aina | Chuo cha Umma |
Chansela | Joan Gabel |
Provost | Joseph J. McCarthy |
Mahali | Pittsburgh, Pennsylvania, Marekani |
Kampasi | Kampasi Kuu, Pittsburgh Kampasi ya Bradford, Kampasi ya Greensburg, Kampasi ya Johnstown, Kampasi ya Titusville |
Rangi | Bluu, Dhahabu |
Msimbo | Panthers (chui mweusi), |
Tovuti | https://www.pitt.edu/ |
Ukweli na Wema |
Chuo kikuu cha Pittsburgh kina shule kumi na saba na wanafunzi elfu ishirini na nane. Kuzungumza kidogo kuhusu historia cha chuo, Chuo Kikuu cha Pittsburgh kilianzishwa mnamo mwaka 1787 kama Akademia ya Pittsburgh.[1] Baadaye, katika mwaka 1819, Jumuiya ya madola ya Pennsylvania ilibadilisha jina la Akademia ya Pittsburgh: Ilitumia jina la Chuo Kikuu cha Magharibi cha Pennsylvania. Hata hivyo, katika mwaka 1845, mji wa Pittsburgh ulishika moto. Baada ya moto, kulikuwa na moto mwingine. Mwishowe, katika mwaka wa 1908, chuo ilikuwa na jina jipya na mahali papya. Kilihamia katika eneo la Oakland kutoka mjini Pittsburgh, na kilipata jina la sasa. Kampasi ya sasa ina ekari 132 na ni sehemu ya Wilaya ya Kihistoria ya shamba ya Schenley.
Chuo Kikuu cha Pittsburgh kimetoa utafiti wa manufaa. Kwa mfano, mwanasayansi mashuhuri Dkt. Jonas Salkaliyetengeneza dawa ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza alipokuwa anafanya kazi hapo chuoni.[2] Katika karne ya 20, ugonjwa wa kupooza ulitishia usalama wa watoto wengi nchini Marekani. Miaka ya 1950, chanjo ya Salk ilishusha haraka haraka tukio la Polio.[2]
Chuo Kikuu cha Pittsburgh kiliwakilishwa na Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Pittsburgh (UPMC). Kilikuwa na madaktari wenye umashuhuri kama Jonas Salk, Peter Safar na Thomas Starzl. Daktari Peter Safar alianzisha mbinu ya matibabu inayoitwa CPR, au ufufuo wa moyo na mapafu. Vilevile, Daktari Thomas Starzl alifanya upandikizaji wa ini wa kwanza wa binadamu. Bila ya serikali, UPMC inaajiri raia wengi wa mji wa Pittsburgh, na Pitt ni ya pili katika hili.[3]
Chuo Kikuu cha Pittsburgh kina shule 17 tofauti. Kina shule ya Sanaa na Sayansi, Biashara (Umahiri), Biashara (shahada ya kwanza), Shule ya Meno, Elimu, Uhandisi, Mafunzo ya Jumla, Sayansi ya Afya, Heshima, Kompyuta na habari, Sheria, Udaktari, Uuguzi, Ufamasia, Masuala ya Umma na Kimataifa, Afya ya Umma, na Kazi za Kijamii.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.