Ana (nabii)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ana (kwa Kiebrania חַנָּה, Hannah, kwa Kigiriki Ἄννα, Anna) alikuwa mwanamke wa karne ya 1 KK katika Israeli.
Ni maarufu kama nabii kutokana na habari iliyomo katika Injili ya Luka (2:36-38[1]).
Humo tunaambiwa kwamba alikuwa binti Fanueli, wa kabila la Asheri.
Alipoachwa mjane ujanani baada ya miaka 7 ya ndoa, alihamia hekalu la Yerusalemu akifunga chakula na kusali hadi miaka 84.[2][3][4][5][6][7][8]
Mtoto Yesu alipoletwa hekaluni siku 40 tu baada ya kuzaliwa, Ana alitangaza habari zake kwa waliokuwepo.
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu nabii.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3[9] au 16 Februari.[10][11]