Yosefu Flavius (jina la awali יוסף בן מתתיהו, Yosef bin Matityahu, 37-100 BK) alikuwa kuhani Myahudi mwenye kujua Kiaramu, Kiebrania na Kigiriki, aliyejipatia umaarufu kama mwanahistoria.

Thumb
Yosefu Flavius.

Maisha

Kwanza alishiriki vita vya ukombozi vya Wayahudi dhidi ya Warumi akishika nafasi ya uongozi huko Galilaya.

Mwaka 67 alisalimu amri akawa mtumwa na mkalimani wa Vespasian kwa miaka miwili.

Huyo alipopata kuwa kaisari alimuacha huru, naye akajiongezea jina Flavius la ukoo wa Vespasian.[1]

Alipata uraia wa Roma, akawa mshauri na mkalimani wa Tito, mwana wa Vespasian, wakati wa kushambulia na hatimaye kuteka Yerusalemu (70).

Maandishi

Vitabu vyake muhimu zaidi vinaitwa kwa Kiingereza The Jewish War (75 hivi) na Antiquities of the Jews (94 hivi).[2]

Cha kwanza kinasimulia vita vya kwanza vya Wayahudi dhidi ya Roma (66-73).

Cha pili kinasimulia historia ya ulimwengu kwa mtazamo wa Kiyahudi lakini namna inayoweza kukubaliwa na Warumi.

Maandishi hayo ni muhimu katika kuelewa Uyahudi wa karne ya 1 na mwanzo wa Ukristo.[2]

Tanbihi

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.