From Wikipedia, the free encyclopedia
Yoana Elizabeti (jina kamili kwa Kifaransa: Jeanne-Élisabeth-Lucie Bichier des Âges; Château des Âges, Poitou, Ufaransa, 5 Julai 1773 – Château des Âges, 26 Agosti 1838) alikuwa bikira ambaye wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa alimsaidia padri Andrea Hubati Fournet kufanya utume wake kwa siri.
Baada ya amani kurudi kwa Kanisa, alimsaidia kuanzisha shirika la kitawa la Masista wa Msalaba, Masista wa Mt. Andrea katika jimbo la Poitiers mwaka 1807 kwa ajili ya kuelimisha fukara na kuhudumia wagonjwa [1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki: Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Mei 1934, halafu Papa Pius XII alimtangaza mtakatifu tarehe 6 Julai 1947.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.