From Wikipedia, the free encyclopedia
Wiski (kutoka Kiingereza: whisky au whiskey) ni kinywaji cha alikoholi kilichotengenezwa kutokana na nafaka kikikaa kuiva katika mapipa ya mbao.
Jina la wiski lina asili katika Kikelti cha Ueire; jinsi ilivyokuwa kote Ulaya, ukenekaji wa maji ya matunda na mchanganyiko wa nafaka na maji uliochachuka ulienezwa na wamonaki, mwanzoni kama dawa, baadaye pia kama kinywaji[1]. Wamonaki waliliita tokeo la ukenekaji kwa Kilatini "aqua vitae" yaani "maji ya uhai" , na "whiskey" ni tafsiri tu ya jina hili katika lugha ya Kikelti ya Ueire[2].
Jinsi ilivyo na vileo vyote vinavyopatikana kwa njia ya ukenekaji, kimiminiko kinachotoka hakina rangi. Wiski inapata rangi yake ya kikahawia kwa kuitunza kwa miaka katika mapipa ya mbao[3].
Wiski hukenekwa kwa usafi wa asilimia 80-94, kutegemeana na sheria za nchi. Baadaye maji yanaongezwa ikiuzwa kwa kawaida ikiwa na kiwango cha alikoholi kisichopungua asilimia 40.
Asili ya wiski ni Ueire na Uskoti. Huko inatengenezwa kwa nafaka ya shayiri. Baada ya kuhamia Marekani, watu kutoka nchi hizo walianza kutengeneza kinywaji kwa kutumia nafaka nyingine kama ngano au mahindi.
Wiski nyingi hutengenzwa Uskoti (inapoandikwa whisky)[4] na Ueire (inapoandikwa whiskey) na kuuzwa kote duniani; katika nchi za Ulaya kuna masharti ya kisheria kuhusu kinywaji kinachouzwa kwa jina wiski.
Wiski za Marekani huitwa "bourbon" kutokana na wilaya ya Bourbon katika Jimbo la Kentucky. Lakini siku hizi hutengenezwa katika nchi nyingi, isipokuwa kuna nchi ambako kile kinachouzwa kama "wiski" ni mchanganyiko wa vileo mbalimbali.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.