Wilaya ya Laikipia ilikuwa moja kati ya wilaya sabini na moja za Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).
Ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa iliyoko kwenye Ikweta.
Makao makuu yalikuwa mjini Nanyuki.
Kwa sasa imekuwa kaunti ya Laikipia.
Wilaya hii ilikuwa na vituo viwili vikuu vya soko: Nanyuki kwenye upande wa kusini mashariki, na Nyahururu kwenye upande wa kusini magharibi.
Wakikuyu walikuwa takribani 60% ya idadi ya watu wote kwenye wilaya hii, huku idadi iliyosalia ikijumuisha watu wa makabila mengine, ni pamoja na Mukogodo Masai, Wasamburu, Wameru, Waborana, Wakalenjin, Wasomali, Wazungu, Watu wa asili ya Asia, na Waturkana, wakiipa wilaya hii idadi ya watu tofauti tofauti. Mashamba mengi yanamilikiwa na idadi ndogo ya masetla wa ukoloni.
Shughuli kuu za kiuchumi katika wilaya hii ni utalii na kilimo, haswa mimea za mbegu, ufugaji na kilimo cha maua,matunda na mboga.
Hali ya hewa ya wilaya hii ni ya baridi kiasi, ikiwa na msimu wa mvua na kiangazi.
Maeneo ya utawala | |||
Tarafa | Idadi ya Watu* | Wakaazi wa mjini* | Makao makuu |
---|---|---|---|
Mkoa wa Kati | 77,478 | 28,489 | Nanyuki |
Lamuria | 38,517 | 0 | Lamuria |
Mukogondo | 13,176 | 624 | |
Ngarua | 65,545 | 2,813 | Kinamba |
Nyahururu | 37,412 | 22,459 | Nyahururu |
Olmoran | 11,069 | 0 | |
Rumuruti | 78,894 | 4,061 | Rumuruti |
Jumla | 322,187 | 58,466 | - |
* 1999 census. Sources: , , |
Wilaya hii ina Majimbo ya Uchaguzi mawili:
- Jimbo la Uchaguzi la Laikipia East
- Jimbo la Uchaguzi Laikipia West
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.