Waborana Oromo (ambao pia huitwa Boran) ni kabila lipatikanalo Kusini mwa Ethiopia, Oromia na Kaskazini mwa Kenya[1] ambao wanajulikana kuwa wafugaji.
Wao ni kundi dogo la Waoromo[2].
Wanawakilisha nusu ya makundi mawili ya Waoromo asili, nusu nyingine ikiwa Wabarentu. Takribani watu milioni 7 wanajitambulisha kama jamii ya Waborana.
Ukweli wa haraka Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana ...
Waborana
Mtu mwenye asili ya Kiborana akipiga kura katika kituo cha upigaji kura Marsabit, Kenya. |
|
Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana |
Ethiopia, Kenya |
Funga
Waoromo wa Kaskazini mwa Kenya waliingia eneo hilo mara ya kwanza kutoka Kusini mwa Ethiopia wakati wa uhamiaji mkubwa wa Karne ya 10.
Walitawanyika kuwa Waborana wafuga ng'ombe na wafuga ngamia, Wagabra na Wasakuye[3].
Waborana huzungumza Kiborana (au afaani Boraana), ambayo ni mojawapo ya Lugha za Kikushi ambayo pia ni mojawapo ya makundi makubwa ya Lugha za Kiafrika-Kiasia.
Inaaminika kuwa Waborana wana Kalenda yao waliyoitunga karibu miaka ya 300 KK. Kalenda yao hutegemea matukio ya anga ya mwezi pamoja na Nyota Saba.
Miezi ya Kiborana (Mizunguko ya miezi na nyota) ni:
- Bittottessa (iangulum),
- Camsa (Pleiades),
- Bufa (Aldebarran),
- Waxabajjii (Belletrix),
- Obora Gudda (Orion-Saiph ikiwa kati),
- Obora Dikka (Sirius),
- Birra (Mwezi mzima),
- Cikawa (gibbous moon),
- Sadasaa (Nusu-mwezi),
- Abrasa (Kipande kikubwa cha mwezi),
- Ammaji (Kipande cha wastani), na
- Gurrandala (Kipande kidogo)[4].
Waoromo wanajumuisha makundi mawili muhimu, ambayo hugawanyika katika koo nyingi za kifamilia.
Kutoka Magharibi kuelekea Mashariki na Kaskazini kuelekea Kusini, matabaka hayo ni:
- Macha Oromo waishio katikati ya mito ya Didessa na Omo, na kusini kuelekea Gibe;
- Tulama Oromo, waishio Oromia, karibu na Addis Ababa;
- Guji Oromo, kundi la Kusini la Waoromo, wanaoishi karibu na Garri na Borana Oromo
- Borana Oromo, waishio katika eneo la Borena Zone, ambayo inajumuisha Moyale. Wanaishi pia nchini Kenya na sehemu za Somalia.
- Gabra Oromo ambao wanaishi Kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Moyale eneo la Garri, (Gharri), ambao wanaishi Kaskazini Mashariki mwa Kenya na sehemu za Somalia
Kuna vikundi vingine vingi pia.
Elliot M. Fratkin, Eric Abella Roth, As Pastoralists Settle, (Springer: 2005), p.39
- Asmerom Legesse, Gada
- Beckingham and G.W.B. Huntingford, Some records of Ethiopia Hakluyt Society, 1954
- Bassi Marco, Decisions in the Shade. Political and juridical processes among the Oromo-Borana Red Sea Press, 2005
- Clifford H F Plowman CMG OBE, Notes On The Gedamoch Ceremonies Among The Boran Archived 15 Julai 2011 at the Wayback Machine., (Journal of the Royal African Society, Vol. 18, No. 70 (Jan., 1919), pp. 114–121 )
- Appiah, Kwame Anthony; Gates, Henry Louis, Jr., whr. (1999), Africana: The Encyclopedia of the African and African American Experience, New York: Basic Books, ISBN 0-465-00071-1, OCLC 41649745
{{citation}}
: CS1 maint: multiple names: editors list (link).
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waborana kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |