Wawindaji-wakusanyaji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wawindaji-wakusanyaji

Wawindaji-wakusanyaji ni jina wanalopewa makundi ya watu wanaoishi bila kuzalisha chakula chao kwa njia ufugaji na kilimo kama ilivyozidi kuwa kawaida ya wengi tangu uzalishaji huo ulipoanza milenia kumi na mbili iliyopita[1].

Thumb
Mwanamume wa Wasan wa Namibia, ambao wengi wao wanaendelea kuwa wawindaji-wakusanyaji.
Thumb
Mgawo wa nyama kati ya Wambendjele.

Kwa kusongwa na wafugaji na wakulima, mara nyingi wawindaji-wakusanyaji wameishia katika maeneo yasiyofaa kwa uzalishaji, wanapoishi kwa kuhamahama, na wametazamwa na kudharauliwa kama watu wasioendelea, ingawa wanaweza kuwazidi wengine kwa maadili[2][3][4][5][6][7][8]

Kwa sababu ya kujali usawa kati yao, Karl Marx aliita mtindo wao wa kuishi Ukomunisti wa awali.[9]

Matarajio ya kuishi ni kufikia kwa wastani umri wa miaka 21-37 tu[10].

Kati ya makabila ya Afrika yaliyo maarufu kwa mtindo huo wa maisha wapo Wahadza wa mkoa wa Singida, Tanzania.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.