Wataita ni kabila nchini Kenya wanaokaa katika kaunti ya Taita-Taveta. Wao huongea Kitaita ambacho ni miongoni mwa lugha za Bantu. Wakiwa Bantu wa Magharibi walihamia wilaya hiyo kwa mara ya kwanza miaka ya 1000-1300 BK[1]

Wataita walihamia Kenya kupitia Tanzania ya leo. Walihamia nchini wakiwa katika makundi matano, kila kundi likifanya makazi katika maeneo tofautitofauti ya kaunti ya sasa ya Taita-Taveta. Walipokuwa wanatulia katika maeneo haya, Wataita walitangamana na makabila mengine, hasa Wataveta, Wapare wa Tanzania, Waborana, Wakamba na Wamasai.

Kuna makabila madogo ya Wataita. Yanaweza kugawanywa katika Wadawida ambao walifanya makazi katika eneo la Dawida, Wasagalla waliotulia katika eneo la Sagalla na Wakasigau waliotulia katika eneo la Kasigau ambalo ni karibu na Milima ya Taita. Wasaghalla huongea Kisagalla, lugha inayokaribiana na Kigiriama au Mijikenda (makabila tisa ambayo huongea lugha zinazokaribiana). Wakasighau hukaribiana na Wapare na Wachagga wa Tanzania lakini ni Wataita.

Kitamaduni, kabila la Wataita lilijumuisha koo (vichuku, kichuku-umoja). Kila ukoo ulikalia sehemu yake katika milima.[2] Kila ukoo ulikuwa kundi lililokuwa na uhuru wake wa kisiasa na kabla ya ukoloni, hapakuwa na wazo la Wataita walioungana.[3]

Siku hizi, lugha ya Wataita (Kidawida, Kitaita) ni lugha iliyojaa maneno ya kukopa kutoka kabila za Wachagga, Wakamba, Wapare, Wamasai, Wakikuyu, Mijikenda na watu wa asili ya Kikushi ambao walitangamana nao.

Kuna pia ufananisho wa majina baina ya Wataita na Wamijikenda na hata Wachagga, Wakamba na makabila mengine. Kwa mfano majina ya Kimijikenda baina ya Wataita ni Kalimbo, Mwatela, Ngao, Chari (ya kisichana) Chaka na mengine mengi.

Katika lahaja, Wataita wana lahaja nyingi sana. Wataita wa Mbololo wana yao, Wataita wa Bura wana nyingine, Wusi, Mghange, Chawia, Mwanda, Kishamba. Hawa ndio wanaitwa Wadawida.

Chakula cha kitamaduni cha Wataita ni Kimanga, ambacho ni chakula cha mihogo na maharagwe. Wataita hujitambulisha sana na jina la ukoo wao (kichuku).

Katika silaha zao, utapata ngao baina ya Wataita wa Mwanda kwa sababu ya utangamano wao na Wamasai isiyokuwa baina ya makundi mengine ya Wataita.

Kuna majina kama abbo, abba ambayo yana asili ya watu wa Kikushi na ambayo yaliazimwa kutoka kwa Waborana walioishi katika sehemu ya Taita nyakati za uhamiaji.

Mwangeka, jasiri anayeenziwa baina ya Wataita, alipinga ukoloni wa Waingereza kukaribia eneo la Wataita.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.