From Wikipedia, the free encyclopedia
Wolfgang wa Regensburg, O.S.B. (934 hivi – 31 Oktoba 994) alikuwa askofu wa Regensburg, Bavaria, Ujerumani, kuanzia Krismasi 972 hadi kifo chake.
Kisha kufanya kazi kama mwalimu wa shule ya kanisa kuu la Trier, halafu kushika maisha ya kimonaki na kupewa upadirisho, alipoteuliwa kuwa askofu, alirudisha nidhamu kati ya wakleri akafa kwa unyenyekevu wakati wa ziara ya kichungaji huko Pupping, leo nchini Austria [1].
Anatazamwa kuwa mmojawapo wa maaskofu bora wa Ujerumani wakati wake pamoja na Ulrich wa Augsburg na Konradi wa Konstanz.
Alitangazwa mtakatifu na Papa Leo IX tarehe 8 Oktoba 1051 na anaheshimiwa hivyo na Waorthodoksi na Waanglikana pia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.