Theodosi wa Kiev
From Wikipedia, the free encyclopedia
Theodosi wa Kiev au Theodosi Pekerski (kwa Kirusi Феодосий Печерский; kwa Kiukraina Феодосій Печерський; Vasylkiv, 1009 - Kiev, 3 Mei 1074) alikuwa mmonaki wa karne ya 11 aliyeleta umonaki wa kijumuia kadiri ya kanuni ya Theodori wa Studion katika sehemu za Kiev (leo nchini Ukraina) na pamoja na Antoni wa Kiev alianzisha monasteri maarufu ya Mapango ya Kiev.

Alitangazwa na Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi kuwa mtakatifu. Anaheshimiwa hivyo na Kanisa Katoliki pia.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Mei[1][2] lakini pia tarehe 14 Agosti.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.