Stefano Kijana

From Wikipedia, the free encyclopedia

Stefano Kijana

Stefano Kijana (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 715 hivi ; Konstantinopoli, 28 Novemba, 764 hivi) alikuwa abati ambaye alidhulumiwa kirefu hadi kuteswa na kaisari Konstantino V wa Bizanti na hatimaye akauawa kwa sababu ya kutetea heshima kwa picha takatifu na imani sahihi [1].

Thumb
Mozaiki ya Mt. Stefano katika monasteri ya Hosios Loukas, Ugiriki.
Thumb
Picha takatifu ya karne ya 1415 kuhusu Ushindi wa Imani sahihi dhidi ya waliopinga heshima kwa picha hizo (843). Mt. Stefano yumo kama mmojawapo kati ya wafiadini wa heshima hiyo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.