Sheria ya kimataifa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sheria ya kimataifa

Sheria ya kimataifa inaweza kuashiria mambo matatu: sheria ya umma ya kimataifa, sheria ya kibinafsi ya kimataifa au mgongano wa sheria na sheria ya mashirika makubwa ya kimataifa, kama vile sheria ya Umoja wa Ulaya.

  • Sheria ya Umma ya Kimataifa inajihusisha na uhusiano kati ya mataifa huru. Vyanzo vya maendeleo ya sheria ya umma ya kimataifa ni desturi, mwenendo na mikataba kati ya nchi huru (Mikataba ya Geneva). Sheria ya umma ya kimataifa inaweza kutengezwa na mashirika ya kimataifa, kama vile Umoja wa Mataifa (ambao ulianzishwa baada ya Shirikisho la Kimataifa kushindwa kuzuia Vita Vikuu vya Pili vya Dunia),[1] Shirika la Kimataifa la Ajira, Shirika la Kimataifa la Biashara, au Shirika la Fedha la Kimataifa.
Thumb
Umoja wa Mataifa ulikubaliwa baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kutoa katiba ya sheria ya kimataifa ya umma.

Sheria ya kimataifa ya umma ina hadhi maalumu kama sheria kwa sababu hakuna kikosi cha kimataifa cha polisi, na mahakama (kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Haki kama tawi la msingi la Umoja wa Mataifa la mahakama) halina uwezo wa kuadhibu wasiotii.[2] Hata hivyo, miundo michache, kama vile WTO, ina mifumo yenye ufanisi ya utatuzi wa kudumu wa migogoro inayoambatana na vikwazo vya kibiashara.[3]

  • Mgongano wa sheria (au "sheria ya kibinafsi ya kimataifa" katika nchi za sheria ya kiraia) unahusisha maeneo ya kimamlaka ya kisheria ya mgogoro wa kisheria baina ya watu binafsi unafaa kusikizwa na sheria za maeneo gani ya kimamlaka ya kisheria ndiyo inayofaa kutumika. Leo, biashara zinazidi kuwa na uwezo wa kusongeza minyororo ya ugavi wa mtaji na ajira kuvuka mipaka, na pia kufanya biashara na kampuni za nchi za ng'ambo, hivyo kulifanya swali kuhusu nchi ipi ndiyo inayo mamlaka ya kisheria kuwa muhimu zaidi. Idadi kubwa zaidi ya biashara zinachagua usuluhishi wa kibiashara chini ya Mkataba wa New York wa mwaka 1958.[4]
  • Sheria ya Umoja wa Ulaya ndiyo ya kwanza, kufikia sasa, ambayo ni mfano wa sheria kuu ya kimataifa. Kutokana na mwenendo wa kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi duniani, mikataba mingi ya kikanda — hasa ya Umoja wa Nchi za Amerika ya Kusini — zimeanza kuufuata mfano kama huu. Katika Umoja wa Ulaya, nchi huru zimekusanya mamlaka yao katika mfumo wa mahakama na taasisi za kisiasa. Taasisi hizi zinapewa uwezo wa kutekeleza kanuni za kisheria dhidi ya au kwa nchi wanachama na raia katika namna ambayo haiwezekani kupitia sheria ya umma ya kimataifa.[5] Kama Mahakama ya Ulaya ya Haki ilivyosema miaka ya 1960, sheria ya Umoja wa Ulaya hujumiusha "muundo mpya wa sheria ya kimataifa" kwa ajili ya faida inayotegemeana ya kijamii na kiuchumi ya nchi zote wanachama.[6]

Tanbihi

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.