From Wikipedia, the free encyclopedia
Saturnini wa Toulouse (kwa Kilatini: Saturninus; kwa Kifaransa: Sernin; Patras, Ugiriki, karne ya 3 - Toulouse, Galia, leo nchini Ufaransa, 257 hivi) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji huo hadi alipouawa katika dhuluma ya kaisari Decius kwa kutoswa chini kutoka kilele cha mwamba ambao Toulouse umejengwa juu yake na ambapo kwanza alikuwa amefungwa na Wapagani. Hivyo alifariki dunia kichwa kikiwa kimepasuka na mwili wote umejaa majeraha [1].
Kadiri ya wanahistoria Wakristo, chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Novemba[2].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.