From Wikipedia, the free encyclopedia
Marsiali wa Limoges (aliishi karne ya 3 BK) alikuwa askofu wa kwanza wa Limoges (leo nchini Ufaransa)[1].
Kadiri ya wanahistoria Wakristo, chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Marsiali huko Limoges[2].
Tangu kale Marsiali anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[3].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.