From Wikipedia, the free encyclopedia
Sanzawa ni kata ya Wilaya ya Chemba katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41811[1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,970 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10613 [3] waishio humo.
Sanzawa ipo katika tarafa ya Kwamtoro. Ina jumla ya vitongoji vinane. Wakazi wake ni wasandawe, wagogo na wabarabaig. Wakazi wa Sanzawa wanajishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, uwele, mtama, udo, mihogo n.k. Mazao ya biashara ni alizeti, ufuta na karanga.
Wakazi wa Sanzawa pia ni wafugaji wa mifugo mbalimbali. Hali ya hewa ya Sanzawa ni nusu jangwa hivyo hukabiliwa na ukame na hali ya ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu. Hivyo kwa wafugaji hutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili mifugo yao.
Sanzawa pia ni makao makuu ya kata. Hivyo ina shule ya sekondari ya kata.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.