Salibu (kwa Kiingereza: en:Crux, au Southern Cross [1]) ni kundinyota mashuhuri yenye umbo la msalaba kwenye angakusi inayoonekana kutoka nusutufe ya kusini ya Dunia. Salibu lipo kati ya kundinyota zinazotambuliwa kirahisi[2]. Ni kundinyota dogo lakini nyota zake kuu zina uangavu mzuri wa mag 2.8 au zaidi.

Thumb
Salibu (en:Crux)
Thumb
Ramani ya Crux - Salibu

Mahali pake

Salibu lipo katika sehemu angavu ya njia nyeupe karibu na Kantarusi (kundinyota) (Centaurus) inayopakana nayo kwa pande tatu. Upande wa kusini lipo Nzi (en:Musca).

Jina

Jina "Salibu"[3] latokana na Kiarabu صليب ṣaliib ambalo ni tafsiri ya kilatini Crux inayomaanisha "msalaba". Jina lilibuniwa na mabaharia kutoka Ulaya walipoanza kuzunguka kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia baada ya safari ya Magellan wakafurahi kuona ishara ya dini yao angani.

Nyota zake zilionekana tayari kwa Klaudio Ptolemaio miaka 2,000 iliyopita akazihesabu kuwa sehemu ya Kantarusi (Centaurus). Kutokana na badiliko la mwelekeo wa mhimili wa Dunia nyota zake hazionekani tena katika nusutufe ya kaskazini. Johann Bayer alipotunga orodha yake ya nyota bado alizieleza kama sehemu za Kantarusi alipomrejelea Ptolemaio. Lakini jina la Crux lilianza kuenea baadaye na kubaki.[4].

Magimba ya angani

Ndani ya eneo la Salibu kuna nyota 49 zinazoonekana kwa macho matupu lakini hasa zile nne angavu zaidi zinazounda umbo la msalaba au "Salibu". Hizi nyota nne zinajulikana kama Acrux, Becrux au Mimosa, Gacrux na Decux ambayo ni mafupisho ya majina marefu yaani Alfa, Beta, Gamma na Delta Crucis.

Gacrux inaonekana kwa darubini ndogo kuwa nyota maradufu lakini hali halisi nyota zake mbili zina umbali wa miakanuru 160 kati yao kwa hiyo zinaonekana tu kama nyota maradufu. Nyota kubwa inayoonekana kwa macho ni jitu jekundu chenye umbali wa miakanuru 88 kutoka Dunia.

Tanbihi

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.