Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
9.14579°S 39.56299°E Kwa kata ya Wilaya ya Muheza fungua Pande (Muheza)
Pande (au Pande Mikoma) ni kata ya Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,038 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,596 [2] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 65409.
Kata ya Pande Mikoma ina jumla ya vijiji 7 ambavyo ni Pande Plot, Nakimwera/Mikoma, Mtitimira, Namwedo, Songo Mnara, Malalani na Nang'oo Kiwala. Kata hiyo inapakana na kata ya Lihimalyao upande wa Kusini, kwa upande wa Kaskazini kuna bahari ya Hindi kuelekea Kilwa Masoko. Upande wa Magharibi kuna kata ya Mandawa na upande wa Mashariki kuna bahari ya Hindi.
Sehemu kubwa ya kata iko barani lakini kuna pia visiwa viwili vya Songo Mnara na Sanji ya Kati. Maghofu ya mji wa kihistoria ya Songo Mnara ni sehemu ya urithi wa dunia wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.
Wakazi wa kata hii ni wa makabila mchanganyiko: wapo Wamwera, Wamalindi, Wangoni, Wayao, Washirazi, Wamakonde na Wanyasa. Kata hii iko mwambao wa bahari ya Hindi, hivyo wakazi wake wana tamaduni za kimwambao. Ni wakarimu sana.
Wakazi wa eneo hilo shuguli zao kuu ni kilimo na uvuvi. Kwa upande wa kilimo wanalima mazao ya chakula ambayo ni muhogo, mtama, mahindi na mpunga na mazao ya biashara ambayo ni korosho na ufuta.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.