From Wikipedia, the free encyclopedia
Panama ni nchi ya mwisho kusini mwa Amerika ya Kati. Shingo ya nchi ya Panama hutazamwa kuwa mpaka kati ya bara la Amerika ya Kaskazini na lile la Amerika ya Kusini.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Latin: Pro Mundi Beneficio (Kilatini: Kwa salama ya dunia) | |||||
Wimbo wa taifa: Himno Istmeño (Wimbo la shingo la nchi) | |||||
Mji mkuu | Panama | ||||
Mji mkubwa nchini | Panama | ||||
Lugha rasmi | Kihispania (rasmi), Kiingereza na lugha za kieneyeji kwenye pwani la Karibi | ||||
Serikali Rais |
demokrasia José Raúl Mulino | ||||
Uhuru kutoka Hispania Kolombia |
28 Novemba 1821 3 Novemba 1903 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
75,517 km² (ya 118) 2.9 | ||||
Idadi ya watu - 2022 kadirio - 2023 sensa - Msongamano wa watu |
3,377,768 (ya 133) 4,064,780 53.9/km² (ya 127) | ||||
Fedha | Balboa (PAB ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-5) (UTC-5) | ||||
Intaneti TLD | .pa | ||||
Kodi ya simu | +507
- |
Imepakana na Kosta Rika na Kolombia; pwani ya Bahari ya Karibi iko upande wa kaskazini na pwani ya Pasifiki upande wa kusini.
Nchi iko kwenye sehemu nyembamba kabisa ya Amerika ya Kati.
Mfereji wa Panama hukata shingo la nchi na kufanya jina la Panama kujulikana kote duniani.
Baada ya ukoloni wa Hispania Panama ilikuwa sehemu ya kaskazini ya Kolombia. Majaribio mbalimbali ya uasi dhidi ya Kolombia kwa shabaha ya kuwa nchi ya pekee katika karne ya 19 hayakufaulu.
Mabadiliko makubwa yalikuja na ujenzi wa mfereji wa Panama.
Utangulizi wake ulikuwa reli kutoka Colon upande wa Karibi kwenda mji wa Panama upande wa Pasifiki iliyojengwa mwaka 1855. Reli hii ilirahisisha safari kati ya Atlantiki na Pasifiki kwa watu na bidhaa kuelekea Kalifornia. Watu wengi walikwenda Kalifornia miaka ile kwa sababu ya dhahabu iliyopatikana kule tangu mwaka 1848 na hapakuwa na reli kati ya pwani zote mbili za Marekani wakati ule.
Wakati wa mwisho wa karne ya 19 Marekani ilianza kujenga mfereji kati ya bahari mbili wa kukata shingo la nchi. Serikali ya Marekani iliona umuhimu wa kutawala njia hii. Ikasaidia Wapanama waliotaka kujitenga na Kolombia kwa kutuma manowari Colon iliyozuia jitihada za Kolombia za kukandamiza ghasia hiyo.
Tarehe 3 Novemba 1903 Panama ilitangaza uhuru wake na kufanya mkataba na Marekani. Panama ilikodisha mlia wa nchi kwa pande zote mbili za mfereji kwa Marekani; Marekani iliahidi kutunza uhuru wa Panama.
Hali halisi ukanda wa mfereji ilikuwa eneo la Kimarekani hadi 31 Desemba 1999 iliporudishwa kwa serikali ya Panama.
Wakazi walio wengi (70%) ni machotara Waindio-Wazungu, 14% wana asili ya Afrika au ni machotara wa Kiafrika, 10% ni Wazungu na 6% Waindio.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.
Upande wa dini, 65-75% ni Wakatoliki na 15-25% Waprotestanti. Nje ya Ukristo, dini kubwa zaidi ni ile ya Bahai (2%).
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Panama kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.