Nungwi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nungwi

Nungwi ilikuwa kata ya Wilaya ya Unguja Kaskazini 'A' katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Tanzania inakadiriwa kupatikana maili 36 (kilomita 56) kaskazini mwa mji wa Zanzibari, katika rasi ya Nungwi, kama mwendo wa saa moja kwa gari kutoka Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Thumb
Mchanga mweupe kwenye ufuko wa bahari wa Nungwi ni kati ya vivutio vya watalii

Postikodi ina namba 73107.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,916 waishio humo. [1]

Nungwi inajulikana pia kama "Ras Nungwi"[2] maana inapatikana kwenye rasi iliyo ncha ya kaskazini ya kisiwa cha Unguja. Katika miaka tangu mnamo mwaka 2000 Nungwi imekuwa moja kati ya vitovu vya utalii vya Unguja.

Ni kijiji kikubwa kinachopatikana kaskazini ya mbali ya visiwa vya Zanzibar ambacho kinaweza kuwa kidogo kuliko eneo la Makunduchi.[3]

Historia

Kulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale katika pwani ya Bahari ya Hindi.

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.