From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto Nile (pia: Naili; kwa Kiarabu: ,النيل an-nīl) ni mto mkubwa upande wa mashariki ya bara la Afrika. Mara nyingi hutajwa kuwa pia ni mto mrefu kabisa duniani kushinda mto Amazonas. Kutoka Ziwa la Viktoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea Nile inavuka nchi za Uganda, Sudan Kusini, Sudan na Misri kwa urefu wa km 6,650.
Nchi za beseni la mto wa Nile pamoja na matawimto yake | |
---|---|
Mto wa Nile | |
Jina: | an-Nil (Kiarabu) |
Mahali: | Africa ya kaskazini-mashariki |
Urefu: | 6650 km |
Chanzo: | Luvironza />mto wa chanzo Burundi |
Kimo cha chanzo: | 2.700 juu ya UB |
Mdomo: | Mediteranea kaskazini ya Kairo/Misri |
Kimo cha mdomo: | 0.00 m juu ya UB |
Tofauti ya kimo: | 2.700 m |
Matawimto ya kulia: | Sobat, Nile ya buluu (Abbai), Atbara |
Matawimto ya kushoto: | Bahr al-Ghazal |
Miji mikubwa mtoni (pamoja na vyanzo vyake): | Alexandria, Assuan, Atbara, Bahri, Fajum, Giza, Jinja, Juba, Kairo, Kampala, Khartum, Kigali, Kusti, Luxor, Malakal, Omdurman, Port Said, Rabak, Tanta |
Je inafaa kama njia ya maji? | ndani ya Misri |
Beseni la Nile hukusanya maji ya eneo linalojumlisha 10% za eneo la Afrika yote au km² 3,349,000. Takriban watu milioni 250 hukalia beseni hilo.
"Nile" au "Naili" ni umbo la Kiingereza la jina la mto lililotokana na lile lililotumiwa na Wagiriki wa Kale: "Neilos" (Νεῖλος). Haijulikani Wagiriki walipata jina hilo kwa njia gani, lakini lilikuwa kawaida nje ya Misri.
Wamisri wa Kale waliita mto huu kwa jina Ḥ'pī au Iteru linalomaanisha "mto mkubwa". Wakopti walikuwa na jina la piaro lakini tangu utawala wa Kiroma jina la Kigiriki lilizidi kutumika, na Waarabu waliendelea na jina la Kigiriki pia, hivyo leo hii wananchi wanasema "an-nil".
Nile ina vyanzo viwili, yaani
Majina hayo ya "nyeupe" na "buluu" yana asili yake katika mji wa Khartoum ambako mito yote miwili inaunganika ilhali kila mmoja una rangi tofauti kutokana na udongo tofauti uliotia rangi yake kwenye maji hayo.
Vyanzo vya Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria Nyanza katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Kenya. Chanzo cha mbali kabisa ni mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika mto Kagera na kufika Ziwa Viktoria Nyanza.
Mkono mwingine wa Nile unaanza Ethiopia ukiitwa Abbai au Nile ya Buluu: unatoka katika Ziwa Tana.
Hakuna mapatano kabisa Nile inaanzia wapi. Kawaida ya waandishi Waingereza ni kuhesabu kuanzia Ziwa Viktoria; waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza wakaita tayari mto Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".
Majina ya sehemu ya mto kuanzia Ziwa Viktoria hadi Khartoum ni kama yafuatayo:
Tangu milenia kadhaa maji ya Nile yamekuwa msingi wa maisha yote nchini Misri na pia kwa sehemu kubwa ya nchi ya Sudan.
Katika miaka ya 1920 Uingereza kama mtawala mkoloni wa Sudan na Misri ulikuwa na majadiliano juu ya ugawaji wa maji ya mto na kufikia mapatano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile ya 1929.
Hadi leo Misri inadai ya kwamba mapatanao yale yanakataa ujenzi wa malambo na kuanzishwa kwa miradi ya umwagiliaji inayotumia maji ya Nile bila kibali cha serikali yake. Hapa Misri inadai ya kwamba nchi zote zilizokuwa makoloni ya Uingereza wakati ule zinafungwa na mapatano ya mwaka 1929 na hizi ni pamoja na Sudan, Uganda, Kenya, Tanzania, halafu pia Ethiopia iliyopatana na Uingereza wakati ule. Nchi nyingine hazikubali madai hayo, ila majadiliano juu ya mapatano mapya ya ushirikiano katika beseni la Nile yanaendelea.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.