From Wikipedia, the free encyclopedia
Nile Nyeupe (kwa Kiingereza: White Nile; kwa Kiarabu: النيل الأبيض, an-nīl al-'abyaḍ) ni mto wa Afrika, moja kati ya matawimto makuu ya Nile; la pili linaitwa Nile ya Buluu. Majina hayo yanatokana na rangi ya maji inayosababishwa na udongo uliomo.[1]
Kwa usahihi, "Nile Nyeupe" ni mto unaopatikana katika Ziwa No, inapokutana mito Bahr al Jabal na Bahr el Ghazal. Kwa maana pana ni mikondo yote inayotokana na Ziwa Viktoria hadi kuungana na Nile ya Buluu. These Mikondo hiyo inaitwa "Nile ya Viktoria" (kupitia Ziwa Kyoga hadi Ziwa Albert), "Nile ya Albert" (hadi mpaka wa Sudan Kusini) halafu "Nile ya mlimani" au "Bahr-al-Jabal" (hadi Ziwa No).[2] "Nile Nyeupe" inamaanisha pengine hata vyanzo vya Ziwa Viktoria.[3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.