From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwada ni kata ya Wilaya ya Babati Vijijini katika Mkoa wa Manyara, Tanzania yenye postikodi namba 27202.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 11,605 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 16,139 waishio humo.[2]
Wakazi wa Mwada kiuchumi wanajihughulisha na masuala ya kilimo cha mazao mbalimbali kama pamba, ufuta, mahindi, ngwara, maharagwe, alizeti na mbaazi, pamoja na uvuvi mdogo katika ziwa Burunge.
Utalii pia ni sehemu mojawapo ya shughuli za kiuchumi katika eneo hilo kutokana na uwepo wa hifadhi ya Burunge ambayo imepakana na hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.