Mwanasiasa wa Kenya na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri From Wikipedia, the free encyclopedia
Wycliffe Musalia Mudavadi (anajulikana zaidi kwa jina la Musalia Mudavadi; alizaliwa katika Kaunti ya Vihiga, 12 Septemba 1960) ni mwanasiasa maarufu nchini Kenya.
'
Musalia Mudavadi | |
---|---|
Mudavadi alitumikia kama Waziri mkuu msaidizi nchini Kenya kuanzia Aprili 2008 mpaka Aprili 2013 | |
Amezaliwa | 12 Septemba 1960 |
Kazi yake | mwanasiasa maarufu nchini Kenya |
Mudavadi amekuwa mbunge kwa miaka mingi. Aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1989 baada ya baba yake, Moses Mudavadi, aliyekuwa akishikilia kiti hicho, kufariki.
Alikuwa ndiye makamu wa rais wa mwisho kabla Daniel Arap Moi hajaondoka madarakani. Inaaminika kuwa alipewa umakamu wa rais ili kushawishi Waluhya kuiunga mkono KANU. Mpango huu haukufanikiwa.
Katika uchaguzi wa urais nchini Kenya mwaka 2002, Mudavadi alikuwa mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta. Pamoja na kuungwa mkono na rais aliyekuwa akimaliza muda wake, Moi, na mtandao mkubwa wa KANU, Kenyatta na Mudavadi walishindwa uchaguzi, Kenyatta hakuchaguliwa kuwa rais na Mudavadi alipoteza kiti cha ubunge wa Sabatia.
Wakati wa upigaji wa kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Kenya, Mudavadi alikuwa kwenye kambi iliyokuwa ikiipinga katiba hiyo. Katika kambi hiyo alikuwemo mwanasiasa maarufu Raila Odinga.
Mudavadi alikuwa kwenye kambi ya watakaogombea urais wa Kenya mnamo Desemba 2007. [1]
Mwaka 2015 alianzisha chama cha Amani National Congress (ANC)[2][3] kilichoendelea kusimama upande wa Raila Odinga kwenye uchaguzi wa rais mnamo 2017.[4]
Mwaka 2021 Mudavadi aliungana na Kalonzo Musyoka (chama cha Wiper), Moses Wetangula (Ford Kenya) na Gideon Moi (Kanu) kuunda ONE KENYA ALLIANCE-OKA kwa kusudi la kumpata mgombea kwenye uchaguzi wa 2022. Mudavadi alitangaza kwamba yeye alilenga kugombea mwenyewe[5].
Tarehe 23 Januari 2022 Mudavadi alimkaribisha makamu wa rais William Ruto kwenye mkutano mkuu wa ANC na hivyo kusababisha wenzake Gideon Moi na Kalonzo Musyoka kuondoka kwenye ushirikiano naye.[6]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.