Atbara (mto)
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Atbara (kwa Kiarabu: نهر عطبرة, Nahr ʿAṭbara) ni tawimto la Nile linalopatikana kaskazini magharibi mwa Ethiopia na katika Sudan.
Chanzo chake ni katika milima ya Simien (Ethiopia) takriban km 50 kaskazini kwa Ziwa Tana au km 30 magharibi kwa mji wa Gondar.
Tawimto lake ni hasa mto Tekeze (Setit) ambao una matawimto mengi. Kiasi cha maji ndani ya Atbara hubadilika sana. Miezi mingi ni mto mdogo sana unaopita katika nchi yabisi lakini wakati wa mvua katika nyanda za juu za Ethiopia unakuwa mpana wenye maji mengi.
Kwenye mji wa Atbara nchini Sudan unaishia katika mto Nile, ukiwa tawimto lake la mwisho kabla ya kufikia Bahari ya Kati.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.