Mto Tekeze
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto Tekezé (pia Täkkäze au Takkaze, kwa Kigeez: ተከዘ au ተከዜ, yaani "mto"; tena: Setit),[1][2] ni mto muhimu wa Ethiopia mpakani mwa Eritrea hadi Sudan.
Una urefu wa kilometer 608 (mi 378) hadi kuungana na mto Atbarah. Umejichimbia bonde linalozidi mita 2,000 (futi 6,562) kwenda chini, hivyo ni refu kuliko yote barani Afrika na kati ya yale marefu zaidi duniani.[3]
Matawimto yake muhimu zaidi ni mto Tahali, mto Meri, mto Tellare, mto Sullo, mto Arekwa, mto Gheoa, mto Wari, mto Firafira, mto Tocoro na mto Gumalo upande wa kulia; halafu mto Nili, mto Balagas, mto Saha, mto Bembea, mto Ataba, mto Zarima na mto Kwalema upande wa kushoto.
Lambo la Tekeze kwa ajili ya uzalishaji wa megawati 300 za umeme[4][5] lilikamilika mwaka 2009
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.