Milima ya Uluguru
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Milima ya Uluguru ni safu ya milima katika Tanzania mashariki, km 200 hivi kutoka Bahari ya Hindi. Ni sehemu ya Milima ya Tao la Mashariki (pamoja na Milima ya Taita nchini Kenya, Milima ya Upare, Milima ya Usambara, Milima ya Unguu, Milima ya Rubeho, Milima ya Ukaguru, Milima ya Udzungwa, Milima ya Uvidunda na Milima ya Mahenge).
Jina limetokana na lile la kabila la Waluguru ambao ndio wenyeji wa eneo hilo.[1] Wakazi wote wa milimani huko ni 151,000.
Milima ya Uluguru ni makazi pekee ya spishi zaidi ya 100 ya mimea, 2 za ndege, 2 za mamalia, 4 za reptilia na 6 za amphibia.
Miinuko ya juu zaidi ni mlima Mtingire na mlima Kimhandu, yote miwili inafikia kimo cha mita 2650 juu ya usawa wa bahari[2].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.