Makazi (kwa Kiingereza na Kilatini: habitat) kwa maana ya elimu ya ekolojia ni eneo au mazingira ambayo ni makao ya mnyama au mmea fulani au aina nyingine ya viumbe hai. Ni mazingira ya asili ambapo kiumbe huishi, au mazingira ambayo yanazunguka idadi ya jamii.
Ufafanuzi
Neno "idadi" huhusishwa na "kiumbe" kwa sababu, inawezekana kuelezea mazingira ya dubu mweusi mmoja, hatuna uwezo wa kutafuta dubu fulani au mmoja lakini kambi ya muungano wa dubu wakati wa kuzaa amabao huwa mahali fulani. Pia, makao hayo huweza kuwa tofauti na makao mengine ya kundi tofauti la dubu weusi. Hivyo, si jamii wala binafsi ambapo jina makazi kutumika.
Makazi madogo
Makazi madogo ni eneo ambalo ni nyumbani mwa viumbe wadogo sana, kama vile chaa wa mbao. Makazi madogo ni makazi ndani ya makazi makubwa, kwa mfano, kuni katika mti ulioanguka. Wadudu huishi kwenye makazi madogo, lakini kipande cha mti kinaweza kuwa makazi madogo kwani nyoka wanaweza kuishi ndani yake. Mazingira madogo ni eneo linalozunguka na masuala ya mmea binafsi au mnyama ndani ya makazi yake.
Makazi ya binadamu
Makazi ya binadamu ni mazingira ambayo binadamu huishi na kuingiliana.
Kwa mfano, nyumba ni makazi ya binadamu, ambapo binadamu hulala na kula.
Aina zake
Kuna makazi ya mjini na makazi ya vijijini.
Makazi ya mjini ni aina ya makazi ambayo watu wanajenga nyumba zao mijini, karibu na wenzao wengi.
Makazi ya vijijini ni aina ya makazi ambayo watu hujenga nyumba zao sehemu za vijijini.
Tazama pia
- Hifadhi ya makazi
- Uharibifu wa makazi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.