Visiwa vya Maluku

From Wikipedia, the free encyclopedia

Visiwa vya Malukumap

Visiwa vya Maluku (kwa Kiingereza: Moluccas) ni kundi la visiwa nchini Indonesia vilivyopo baina ya Sulawesi na Guinea Mpya.

Thumb
Ramani ya Maluku; Maluku Utara = Maluku Kaskazini

Eneo lote la Maluku ni takriban kilomita za mraba 850,000 lakini nchi kavu yaani visiwa vyenyewe ambavyo ni 1,027 ni km² 74,505 pekee.

Wakazi ni takribani milioni 2.8.

Maluku ilikuwa jimbo la Indonesia hadi mwaka 1999 lilipogawiwa kuwa majimbo mawili

Visiwa vya Maluku vilijulikana kama "Visiwa vya viungo" (Spice islands) na Waarabu, Wareno na Waholanzi walishindana hapa kutawala biashara miaka 500 iliyopita hadi Maluku pamoja na visiwa vingine vya Indonesia vilipata kuwa koloni la Uholanzi.

Hadi leo kilimo cha karafuu na kungumanga ni muhimu kiuchumi pamoja na uvuvi.

Wakazi ni mchanganyiko hasa wa Wamalay pamoja na Wamelanesia. Upande wa dini Wareno walifaulu kuvuta wenyeji wengi upande wa Ukristo ilhai sehemu nyingine za Indonesia walihamia zaidi Uislamu lakini juzijuzi watu wengi walifika kutoka pande nyingine za Indonesia, wengi wao wakiwa Waislamu.

Baina ya mwaka 1999 na 2002 kulikuwa na mapigano baina ya Wakristo na Waislamu: maelfu walipoteza uhai na takriban nusu milioni walifukuzwa kutoka makazi yao.

Tanbihi

Marejeo

Kujisomea

Viungo vya Nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.