Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nathaniel Thomas Wilson (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Kool G Rap, kwa kifupi G Rap, Kool G. Rap, na Giancana, iliyo maana ya kifupisho "G."; amezaliwa 20 Julai 1968[1]) ni rappa, kutoka mjini Corona jirani na mji wa Queens, New York huko nchini Marekani.[2] Ameanza shughuli zake za kurap katikati mwa miaka ya 1980 akiwa kama nusu ya kundi la Kool G Rap na DJ Polo na pia akiwa kama mwanachama wa Juice Crew.
Kool G Rap | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nathaniel Thomas Wilson |
Amezaliwa | 20 Julai 1968 Queens, New York City, U.S. |
Asili yake | Corona, Queens, New York City, U.S. |
Aina ya muziki | Hip hop, mafioso rap, hardcore hip hop |
Kazi yake | Rapa, mtayarishaji wa rekodi, mwandishi-skrini, mtunzi wa vitabu |
Miaka ya kazi | 1986–hadi sasa |
Studio | Cold Chillin'/Warner Bros. Records Cold Chillin' Cold Chillin'/Epic Street/SME Records KOCH' |
Ame/Wameshirikiana na | DJ Polo, Juice Crew, Marley Marl, Big Daddy Kane, Rakim, Canibus, Five Family Click, Wu-Tang Clan, Nas, MF Grimm, Mobb Deep, R.A. The Rugged Man, Ras Kass, DJ Premier, Rick Ross |
Mara kwa mara huhesabiwa kama miongoni mwa Ma-MC wenye athira na maarifa ya juu wa muda wote[3][4][5][6][1][7][8]akiwa kama mwanzilishi wa staili ya mafioso rap/street/hardcore[5][9][10][11][12][13] na uimbaji wa silabinyinginyingi.[14] Kwenye albamu yake ya The Giancana Story, ameeleza ya kwamba herufi "G" katika jina lake humaanisha "Giancana" (kajipa jina la jambazi sugu Sam Giancana), lakini kwa namna nyingine mwenyewe eti anadai lina-maanisha "Genius".[1]
Pia amewahi kutajwa na wasanii maarufu wa hip hop kama vile Eminem, Nas, Jay Z, Big Pun, RZA na wengine wengi tu.[15][16][17]
Wilson amekulia katika mazingira hafifu mno huko mjini Corona Queens, New York akiwa na mtayarishaji mkongwe Eric B.[18] Katika mahojiano yake na jarida la The Source alieleza;
“ | Kukulia mjini Corona ilikuwa kama Harlem ndogo, haikuwa vigumu sana kwa mtu mweusi kujihusisha na maisha ya mtaa hasa yale ya uendawazimu. Wakati nilivyokuwa kama na umri wa miaka 15 hivi, washikaji zangu hawakuweza kuvaa nguo nzuri na kwa kipindi hicho lazima utahitaji uwe na kiasi fulani cha pesa mfukoni mwako. Hicho ndicho kilichotukumba sisi sote, kulewa na mambo mabaya. Watu weusi wanashikwa na uchizi. Watu weusi wanaanza kuuza dawa za kulevya vichochoroni, na mambo hayo yote, ndiyo mambo yaliyokuwa yakiendelea huko mitaani... hatimaye maswahiba zangu wote wakawa wavutaji. Kila mtu alikuwa anadondoka kimaisha'. Maswahiba zangu wote wakaanza kufungasha vipuli vya bangi kila siku, kwa kifupi tulichizika kwa sana.[19] | ” |
Wakati fulani, Wilson alikuwa anamtafuta DJ, na kwa kupitia Eric B., akakutana na DJ Polo, ambaye alikuwa anamtafuta MC wa kushirikiana nae.[18]
na DJ Polo | Mwaka |
---|---|
Road to the Riches | 1989 |
Wanted: Dead or Alive | 1990 |
Live and Let Die | 1992 |
Albamu za Kujitegemea | Mwaka |
4,5,6 | 1995 |
Roots of Evil | 1998 |
The Giancana Story | 2002 |
Half a Klip | 2008 |
Riches, Royalty, Respect | 2011[20] |
Kompilesheni | Mwaka |
Killer Kuts | 1994 |
Rated XXX | 1996 |
The Best of Cold Chillin' | 2000 |
Greatest Hits | 2002 |
Kool G Rap & Twinn Loco Present – I Live Hip Hop – The Mixtape | 2010 |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.