From Wikipedia, the free encyclopedia
William Michael Griffin Jr. (alizaliwa 28 Januari, 1968), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Rakim (/rɑːˈkɪm/), ni rapa kutoka nchini Marekani. Ni msanii mwenza wa enzi za kizazi cha dhahabu cha hip hop—Eric B. & Rakim, ambao walitoa albamu nne: Paid in Full (1987), Follow the Leader (1988), Let the Rhythm Hit 'Em (1990), na Don't Sweat the Technique (1992). Pia ametoa albamu nne kama msanii wa kujitegemea: The 18th Letter (1997), The Master (1999), The Seventh Seal (2009), na G.O.D.'s Network: Reb7rth (2024).
Rakim | |
---|---|
![]() Rakim akitumbuiza mnamo 2008 | |
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | William Michael Griffin Jr. |
Pia anajulikana kama | The God MC, Kid Wizard, The R, The 18th Letter, Rakim Allah |
Amezaliwa | 28 Januari 1968 Wyandanch, New York, U.S. |
Kazi yake | Rapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi |
Eric B. & Rakim |
Rakim huhesabiwa kama mwanampinduzi hip hop kwa kusogeza mbele mbinu za MC kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa hapo awali. Alisaidia kuanzisha matumizi ya mizani ya ndani (internal rhymes) na mizani yenye silabi nyingi (multisyllabic rhymes). Rakim alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kuonyesha uwezo wa kuandika mashairi yaliyochongwa kwa ustadi. Mashairi yaliyojaa maneno ya busara na tamathali za semi, badala ya kutumia mitindo ya uchanaji wa kujirudiarudia na mifumo rahisi ya mizani iliyotawala kabla yake.[1] Pia anapewa sifa kwa kuleta mabadiliko kutoka kwa mitindo rahisi ya awali ya hip hop hadi mitiririko tata zaidi.
Rapa Kool Moe Dee alieleza kuwa kabla ya Rakim, neno flow (kughani) halikutumika sana – "Rakim kimsingi ndiye mvumbuzi wa flow. Hatukuwa tunatumia neno hilo kabla yake. Ilikuwa inaitwa uchanaji wa mashairi (rhyming), au mpangilio wa midundo (cadence), lakini haikuitwa flow. Rakim alibuni flow!"[2]
Albamu Paid in Full ilitajwa kuwa albamu bora zaidi ya hip hop ya wakati wote na MTV mnamo 2006, huku Rakim mwenyewe akishikilia nafasi ya nne kwenye orodha ya MTV ya MC wakubwa wa muda wote.[3] Steve Huey wa AllMusic alisema kuwa "Rakim anaheshimiwa karibu na kila mtu kama mmoja wa MC bora zaidi – labda bora zaidi – wa wakati wote ndani ya jamii ya hip hop." Wahariri wa About.com walimuweka nafasi ya pili kwenye orodha yao ya Top 50 MCs of Our Time (1987–2007). Mnamo 2012, The Source ilimuweka namba moja kwenye orodha yao ya Top 50 Lyricists of All Time.[4]
Albamu za kujitegemea
With Eric B. & Rakim
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.