From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibungo (au Kibungo Juu) ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67228.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,892 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,304 [2] walioishi humo.
Kata ya Kibungo juu inaundwa na vijiji vitano navyo ni: Kibungo Juu, Lanzi, Nyingwa, Dimilo na Lukenge. Kuna shule za msingi tano, moja kwa kila kijiji.
Wananchi wa kata ya Kibungo ni wakulima wa mazao ya biashara kama vile karafuu, hiriki, tangawizi, bizari, ndizi, lakini wanalima pia mazao ya chakula kama vile mpunga, mahindi, mihogo, magimbi na mengineyo.
Tamaduni za wananchi wa Kibungo Juu hazina tofauti na zile za Waluguru wengine; kwa uchache ni wakarimu na wanaheshimu akina mama; ndiyo maana ukoo unakwenda kwa kufuata mama.
Kiimani wananchi wa kata hiyo wamegawanyika katika dini kubwa mbili: Waislamu na Wakristo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.