Kaunti ya Turkana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaunti ya Turkana ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Turkana | |
---|---|
Kaunti | |
Mto Turkwel ukiwa umekauka wakati wa ukame | |
Kaulimbiu: "" | |
Turkana County in Kenya.svg![]() Kaunti ya Turkana katika Kenya | |
Coordinates: 3°09′N 35°21′E | |
Nchi | Kenya |
Nambari | 23 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Bonde la Ufa |
Mji mkuu | Lodwar |
Miji mingine | Lokichogio, Kakuma, Lokichar |
Serikali | |
Gavana | Jeremiah Napotikan |
Naibu wa Gavana | Peter Lotethiro Emuria |
Seneta | James Lomenen |
Mwakilishi wa wanawake | Joyce Akai Emanikor |
Bunge | Bunge la Kaunti ya Turkana |
Wawakilishi Wadi | 30 |
Maeneo bunge | 6 |
Eneo | |
Jumla | km2 68 232.9 (sq mi 26 344.9) |
Idadi ya Watu | |
Jumla | 926,976 |
Msongamano | 14 |
Majira ya Saa | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti turkana.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 926,976 katika eneo la km2 68,232.9 msongamano ukiwa hivyo wa watu 14 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Lodwar.
Jiografia
Kaunti ya Turkana ndio kaunti kubwa zaidi ikiwa na km2 71 597.8 (sq mi 27 644.1). Imepakana na Uhabeshi, Sudani Kusini (kaskazini), Uganda (magharibi), Pokot Magharibi, Baringo, Samburu (kusini) na Marsabit (mashariki).
Turkana ina safu za milima: Milima Loima, Milima Lorengippi, Milima Mogila, Milima Songot, Milima Kalapata, Milima Loriu, Milima Kailong’kol na Milima Silale. Safu hizo ni vyanzo vya maji. Vilima vya Tepes, Vilima vya Lokwanamoru, Vilima vya Lorionotom, Vilima vya Pelekech na Vilima vya Loima pia hupatikana katika Turkana[2].
Tambarare za kaunti hupatikana katika sehemu kavu za kaunti.
Mto Tarach, Mto Kerio, Mto Kalapata, Mto Malimalite na Mto Turkwel ndio mito mikuu katika kaunti. Mito hii hupungua kiwango cha maji msimu wa kiangazi, na kukauka wakati wa ukame[3]. Ziwa Turkana liko mashariki mwa kaunti. Limegawanywa kati ya Turkana, Marsabit na Uhabeshi. Katika maeneo karibu na ziwa, kuna chemchemi zilizopo. Chemchemi za Eliye ndio chemchemi maarufu na kivutio cha watalii[2].
Turkana ina tabianchi kavu na nusu kavu. Kaunti hupata misimu miwili ya mvua: Aprili hadi Julai na Oktoba hadi Novemba[2].
Utawala
Kaunti ya Turkana imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[4]:
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [5]
- Kibish 36,769
- Loima 107,795
- Turkana Central 185,305
- Turkana East 138,526
- Turkana North 65,218
- Turkana South 153,736
- Turkana West 239,627
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.