mwanamuziki wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Juma Nature au Sir Nature (alizaliwa kama Juma Kassim Ally huko Dar es Salaam, 1980) ni mwanamuziki wa aina ya Bongo Flava na Hip Hop kutoka Tanzania. Ni mwanzilishi wa kundi la TMK.
Juma Nature | |
---|---|
Juma Nature | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Juma Kassim Ally |
Pia anajulikana kama | Sir. Nature Kibla Msitu wa Vina Jitu la Maneno ya Shombo |
Amezaliwa | 1980 |
Kazi yake | Rapa |
Miaka ya kazi | 1997 - hadi leo |
Studio | Bongo Records Sound Crafters Records Mj Records |
Ame/Wameshirikiana na | Dknob Mh Temba Dark Master TID Solo Thang Professor Jay AY Inspector Haroun Chegge Mandojo na Domokaya Zay B. |
Nature ni msanii mbunifu: si mtunzi tu; pia ana kipaji cha kujaliwa na sauti nzuri ya uimbaji. Sababu nyingine zipelekeazo muziki wa Juma Nature upendwe Afrika Mashariki ni mashairi anayotunga. Baadhi za nyimbo zilizompa heshima kitaifa ni ile ya 'Umoja wa Tanzania' ambayo yenyewe ilikuwa inataka kupatanisha mgogoro wa kisiasa kati ya vyama vya CCM na CUF. Hakuishia hapo, zipo nyimbo nyingine nyingi tu zenye kutoa husia kwa Taifa. [1][2]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.